Muigizaji Irene Uwoya amemshukuru Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa
kuwathamini na kuwaamini wanawake kwa kuwapa nafasi za juu katika
kuongoza taifa la Tanzania.
Uwoya kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa hawezi
kumsahau Rais huyo kutokana na uamuzi wake wa kutoa nafasi kubwa kwa
wanawake katika serikali yake, zikiwemo nafasi za uwaziri, majaji na
hata Spika wa bunge, na kwamba, Rais huyo ndiye aliyempa motisha ya
kugombea ubunge.
“Namshukuru sana Rais mstaafu… Mh. JAKAYA MRISHO KIKWETE kwa kutupa
wanawake heshima na kututhamini… Alitupa nafasi nyingi sana katika
nafasi za mawaziri, majaji na spika… Na hata mimi kama msanii
nilihamasika na kuona naweza kugombea ubunge… Kiukweli amefungua njia na
ameweka mwanga mkubwa kwa viongozi wengine na wao wakaendelea kuthamini
na kuheshimu mchango wetu katika jamii ndiyo maana hata tukapata makamu
wa Rais mwanamke kwa mara ya kwanza Tanzania”. Amesema Irene
Katika hatua nyingine, Uwoya ameungana na wanawake wengine duniani
kusherehekea siku ya wanawake, huku akionesha kukerwa na wanaume
wanaowadharau wanawake huku akiongeza kuwa wanawake wana mchango mkubwa
katika jamii na kwamba mwanamke ni mlezi na pia wakati mwingine husimama
kulisha familia.
“Mwanamke ndiye mama wa taifa… Ndiyo maana Marekani mwaka 1911
iliadhimishwa siku ya wanawake duniani ambapo vikundi tofauti vya
wanawake viliungana kupinga ukandamizaji, uonevu na ubaguzi wa jinsia
hususani sehemu za kazi… ” Ujumbe wa Irene Uwoya.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment