ongea na mwanao ni kampeni iliyoendeshwa kipindi cha uchahuzi wa rais 2015, ambapo wasanii mbalimbali waliungana kupigania chama cha Mapinduzi CCM, Steven Nyerere akisaidiana na Wema Sepetu wakiwa viongozi wa kampeni hiyo walizungunguka nchi zima kupigania CCM kuendelea kuwa madarakani.
Katika kampeni hiyo kila msanii alihaidiwa kulipwa laki tano mara
baada ya kumaliza kuzunguka kila mkoa mmoja, lakini kwa baadhi ya
maelezo ya wasanii mara tu baada ya kumaliza mkoa mmoja hawakuweza
kukabidhiwa fedha zao walizoahidiwa kabla ya kampeni.
Utata umezuka katika wasanii walioshiriki kampeni ya mama ongea na
mwanao kwani wasanii hao wametengeneza tabaka wapo wanaodai kulipwa
fedha zao pia wapo wanaodai kutolipwa fedha zao.
Hivyo baadhi ya wasanii wameungana na kumtaka mchekeshaji Steve
Nyerere kuonesha mkataba wa malipo ambao ulitolewa na CCM lengo kubwa
ni kukata mzizi wa fitina baina ya wasanii, wananchi na uongozi mzima wa
CCM.
Pia wameomba Viongozi wa CCM kumbana Steve Nyerere, aeleze ni wapi
fedha za wasanii hao alikozipeleka kwa sababu kitendo cha kudhulumu
fedha hizo baadhi ya wananchi wanafikiri kimefanywa na chama cha
mapinduzi CCM wakati mzigo wote ulikabidhiwa kwa Steve Nyerere.
Steve alikua na la kujibu kuhusiana na tuhuma hizo na kudai kuwa
wote ambao hawakulipwa fedha taslimu ni wale ambao walikuwa hawana
mkataba ni wabeba mizigo .
‘’Alikwambia ana mkataba, huyo alikuwa hakuajiriwa na alikuwa mbeba
mizigo na wabeba mizigo wote wameshalipwa hakuna anayedai ‘’.
Hivyo Nyerere aliwaomba wananchi kupuuzia tuhuma hizo kwani hazina ukweli ndani yake.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment