Kada wa Chadema katika Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, Anitha Swai ameuawa katika tukio lililogubikwa na wingu zito.
Taarifa za awali zilizopatikana usiku huu zimedai kuwa Anitha ambaye
aligombea ubunge wa viti maalum mwaka 2015, alitekwa nyara wilayani
Rombo na kuuawa maeneo ya TPC nje kidogo ya mji wa Moshi.
Vyanzo mbalimbali vya habari vimedokeza kuwa mara ya mwisho mwanasiasa
huyo alionekana akiwa na watu wawili wilayani Rombo siku ya Jumatatu,
Februari 27 na kuaga wanaelekea Arusha.
Hata hivyo, tangu siku hiyo Anitha hakuonekana hadi maiti yake
ilipogunduliwa leo (Alhamisi) jioni maeneo ya TPC huku gari lake likiwa
limetelekezwa maeneo ya Bomambuzi mjini Moshi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha
kuokotwa kwa mwili huo, lakini amekataa kuthibitisha kama ni wa kada
huyo wa Chadema.
"Ni kweli kuna tukio hilo, lakini ninachoweza kusema bado hajatambuliwa
na mwili wake umepelekwa KCMC ili ndugu waweze kuutambua," amesema.
Hata hivyo, Diwani wa Viti Maalumu wa Kata ya Mawenzi mjini Moshi, Hawa
Mushi amethibitisha kuwa aliyeuawa ni kada wa chama chao, lakini chanzo
na nani waliohusika hakijajulikana.
Hawa amesema taarifa zilizothibitishwa ni kuwa mwili wake ulipatikana
maeneo ya TPC huku simu iliyopatikana katika gari yake ndiyo iliyosaidia
kumtambua.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment