Friday 18 March 2016

JOKATE : NASUBIRI LOWASA KURUDI CCM.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Baada ya Balozi Juma Mwapachu leo kutangaza kurudi CCM, miezi mitano tangu akihame chama hicho na kuunga mkono upinzani, mwana mitindo maarufu na mjasiriamali wa Tanzania Jokate Mwegelo amefunguka na kusema anasubiri sasa Lowassa kurudi chamani.


Kupitia account yake ya twitter Jokate ameandika ujumbe mfupi na kusema anasubiri EL kurudi chamani "Waiting on EL kurudi chamani".


Ujumbe huu wa Jokate umekuja masaa machache baada ya Balozi Mwapachu kutangaza kurudi rasmi leo katika chama chake hicho cha CCM na jambo hili limepokelewa tofauti na baadhi ya mashabiki wa ukurasa wa facebook wa East Africa Radio, wapo wanaompongeza na wapo wanaombeza.


"Huyo CCM mwogopeni kama ukoma, tatizo lake anahangaika kutafuta madaraka, anasaliti huku na huku ndio wanaosababisha uhasama katika nch,inatakiwa achukiwe kila mahali" aliandika Daud Mwakyeja.


Na upande wake Emmanuel Mwakyusa alikuwa na haya ya kusema "Duuuuu angekuwa baba yangu ningemwambia kitu kwa vile sio nampotezea, msomi mzima kubadili msimamo miezi miwili ni aibu hana uzalendo wala thamani ya uelewa tuwakatae kina Mwapachu hawana msaada 'Edo' inaonekana thabiti hajarudi nyumba kuliko Mwapachu".


0 comments:

Post a Comment