Wednesday 16 March 2016

#YALIYOJIRI>>> Mkuu Mpya Wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu Atoa Onyo Kali Kwa Majambazi na Wahalifu.Fahamu zaidi hapa.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu amewataka watu wote wanaopindisha sheria, majambazi na wahalifu wote kutafuta kazi nyingine halali za kufanya.

Meja Kijuu aliyasema hayo baada ya kula kiapo cha utiifu na uadilifu kuwatumikia wananchi wa mkoa wa Kagera mkoa ambao upo pembezoni mwa nchi unaokabiliwa na matukio ya mara kwa mara ya uhalifu.

''Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa imani kubwa aliyonayo kwangu na nitafanya kazi kwa kuzingatia yale ambayo ameyasema na kuhakikisha maendeleo yanapatikana''-Amesema Meja Kijuu

''Sitakubali watu wazurure hovyo na kuacha kufanya kazi za uzalishaji na nitahakikisha napambana na wahalifu wote kwa uwezo wote nilionao"-Amesisitiza Meja Kijuu.

Aidha Rais Magufuli aliwaapisha wanajeshi wastaafu Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Elias Kyunga, aliyekuwa Chuo cha Kamanda na Unadhimu (JWTZ) ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu, aliyekuwa Mkuu wa Kamandi ya Nchi Kavu ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Wengine ni Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga, aliyekuwa Makao Makuu ya Jeshi sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma lengo la Rais kuweka wanajeshi katika mikoa ya pembezoni ni kuleta usalama na kuimarisha amani katika mikoa hiyo.

0 comments:

Post a Comment