Friday 11 March 2016

#YALIYOJIRI>>>Serikali Yakifunga Chumba cha Maiti Tumbi.Fahamu zaidi hapa.

Serikali imefunga kwa siku tatu Chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya rufani ya Tumbi Mkoani Pwani kutokana na hali mbaya ya chumba hicho ukiwamo ubovu wa majokofu na huduma isiyoridhisha.

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara hiyo Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinisia, Wazee na Watoto Mhe. Khamis Kigwangala amesema amechukua uamuzi huo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa msimamizi wa chumba hicho.

Naibu waziri amesema amekuta changamoto kadhaa katika chumba hicho ikiwemo ubovu huo wa Mjaokofu hali inayosababisha maiti kulazwa sakafuni, na kupelekea kuharibika na kutoa harufu kali.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kigwangala amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Elimu Kibaha kuandika barua ndani ya msaa 24 ya kujieleza kwanini asifukuzwe kazi kutokana na kushindwa kutatua changamoto zinazoikabili hosptali teule ya Tumbi.

Naibu Waziri huyo amesema amebaini kuwa kuna tatizo la kiutawala hali inayosababisha utoaji wa huduma za kimatibabu kuwa wa kusuasua ikwamo kukosekana kwa maji,ubovu na uchakavu wa chumba cha upasuaji, ukosefu wa dawa na chupa za kuhifadhia damu.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa na uongozi wa Hospitali hiyo akiwemo Mganga Mkuu wa Hospitali, Dk. Peter Datani (kulia) akitembelea katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi wakati wa ziara hiyo mapema jana Machi 10.2016.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla alipowasilia kwenye Mochwari hiyo wakati wa ukaguzi huo katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi, mapema jana Machi 10.2016.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua Mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa agizo hilo kwa uongozi wa Hospitali hiyo pamoja na viongozi wa Serikali juu ya kuifunga Mochwari hiyo kwa siku tatu hadi hapo itakapofanyia ukarabati mambo mbalimbali yanayoikabili Mochwari hiyo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia kifaa maalum ndani ya Mochwari hiyo ambapo hata hivyo hakifanyi kazi.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua Mochwari hiyo. Ambapo hadi sasa licha ya matatizo inayoikabili mochwari hiyo haina umeme na vifaa muhimu ikiwemo kipima cha kupimia joto kuharibika.

0 comments:

Post a Comment