Monday 14 March 2016

#MICHEZO>>>SIMBA YAONYESHA UBABE TAIFA, AWADH JUMA SHUJAA.FAHAMU ZAIDI HAPA.


Awadh Juma (katikati) akisujudu baada ya kupachika bao lililoipa Simba ushindi
Bao pekee lililoipa pointi tatu Simba limewekwa kambani dakika ya 86 na kiungo Awadh Juma kwa shuti kali akiwa nje ya box la 18 na kupeleka shangwe mtaa wa Msimbazi, Kariakoo.
Awadh Juma (mbele) akipongezwa na wachezaji wenzake Mussa Mgosi (kulia) na Danny Lyanga (kushoto) baada ya kuifunga bao lililoipa Simba pointi tatu
Simba bado imeendelea kutamba kwenye ligi ya Vodacom Tanzania bara baada ya kuinyamazisha Tanzania Prisons ya Mbeya kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa raundi ya pili ya ligi uliochezwa kwenye uwanja wa taifa.

0 comments:

Post a Comment