Wednesday 23 March 2016

#YALIYOJIRI>>>>Wananchi Mwanza waandamana kupinga kuuzwa kwa Mlima wa Buyombe.Fahamu zaidi hapa.

Mamia ya wakazi wa mtaa wa Buyombe Kata ya Kahama jijini Mwanza wakiwa na silaha za jadi,wameandamana kupinga vikali kuuzwa kwa Mlima wao kunakodaiwa kufanywa na baadhi ya watumishi wa idara ya ardhi na mipango miji ya jiji hilo kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya chuo cha elimu ya biashara,kampasi ya Mwanza huku baadhi yao wakionyesha hasira zao baada ya kuanza kung’oa vigingi vyote pamoja na mabango ya Chuo hicho.

Wakazi hao wanasema kuwa hawako tayari kuchangia shilingi elfu hamsini kwa kila kaya kwa ajili ya ujenzi wa shule yao ya msingi kwani zaidi ya shilingi milioni mia sita zilizotokana na mauzo ya mlima huo kwa chuo cha elimu ya biashara kampasi ya Mwanza pamoja na wananchi wengine zinatosha kabisa kugharimia miundombinu ya huduma za kijamii kama vile shule,zahanati,maji ya bomba na Barabara.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Buyombe,Emanuel Zambezi amesema madai ya wakazi hao yana mantiki kubwa.

0 comments:

Post a Comment