Wednesday 16 March 2016

#YALIYOJIRI>>>Uchomaji Kituo cha Polisi Bunju A....Watuhumiwa 17 Waachiwa huru.Fahamu zaidi hapa.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru washtakiwa 17 kati ya 35 wanaokabiliwa na kesi ya kuchoma moto Kituo cha Polisi Bunju ‘A’ baada ya Upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka

Hukumu hiyo imetolewa mahakamani hapo na Thomas Simba, Hakimu Mkazi huku upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Hellen Moshi, Wakili wa Serikali.

Katika kesi hiyo, Hakimu Simba amesema hatua hiyo inatokana na upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao wakiwa na mashahidi 17 pamoja na vielelezo 19.

Amesema, kutokana na kushindwa kuthibitisha mashtaka kwa washtakiwa 17 mahakama imeamua kuwaachia huru kwa kuwa hawana hatia, huku washtakiwa waliobaki 18 wakipatikana na kesi ya kujibu.

Washtakiwa walioachiwa ni Halifan Mshengeli, Patrick Elias, Jacob Kasambo, Amos Machaka, Hamis Mohamed, Elia Nalomba, Juma Kapanga,

Wengine ni Josephine Machimo, Shadya Ismail, Aisha Husseion, Jenerose Urio, Suzan Shaulin, Mariam Mwinyi, Madgalena Nashokigwa, Mariam Rashid, Pili Ally na Said Mwindi.

Washtakiwa ambao wamepatikana na hatia baada ya kutolewa kwa ushahidi ni Yusuph Sungu, Juma Koza, Rashid Liwima, Mrisho Majaliwa, Hamis Ndege, Seleman Gwae, Baraka Nkoko, Mang’ enya Mang’enya.

Wengine ni Abuu Issa, Ramadhan Said, Rajab Ally, Ally Athuman, Abraham Nunge, Amina Matipwili, Mariam Hoza, Rehema Juma, Gudila Temba,  Veronica Ephraem (Mama Wambura).

Hakimu Simba amesema, washtakiwa hao wamepatikana na kesi ya kujibu katika mashtaka sita yanayowakabili, hivyo kutokana na wingi wa wananchi kesi hiyo itasikilizwa siku mbili mfululizo kuanzi Machi 29 hadi 30, mwaka huu kwa ajili ya kujitetea.

Baada ya kusema, hayo kuliibuka hoja za kisheria kati ya Wakili Moshi na wakili wa utetezi Felix Nkongwa kuhusu kupata dhamana kwa washitkiwa waliobaki.

Kutokana na mvutano wa hoja, Hakimu Simba amesema uamuzi wa kupata ama kutopata dhamana kwa washitakiwa hao utatolewa Machi 22, mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment