Thursday 13 July 2017

Kimenuka..Ofisi ya CCM Yachomwa Moto Pwani.

Watu wasiojulikana wameichoma moto ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) tawi la Mshonzini iliyopo Wilayani Mafia Mkoani Pwani na kuteketeza mali mbalimbali za chama hicho.

Katibu wa CCM Wilayani Mafia, Mohammed Dhikiri, amethibitisha kutokea kwa tukio na kusema ofisi hiyo imechomwa moto usiku wa kuamkia leo na kuongeza kuwa moto huo umeteketeza kabisa ofisi hiyo na samani za ndani.

Bw. Mohammed amesema bado haijajulikana sababu za ofisi hiyo kuchomwa moto kwa kuwa wakati tukio linatokea hakukuwepo na viashiria vyovyote vya vurugu miongoni mwa wanachama wa chama hicho.

Naye Mbunge wa Mafia, Mbaraka Dan, amesema, vipo viashiria vinavyoonesha kuwa alifika mtu asiyejulikana karibu na ofisi hiyo kisha kuwasha na kurusha kijinga cha moto kwenye paa la makuti la ofisi hiyo na kwamba, mtu huyo baada kutekeleza kitendo hicho aliondoka kuelekea kichakanani kama ambavyo alama za nyayo za miguu yake zinavyoonesha.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment