Tuesday 11 July 2017

USAJILI: Singida United yafunga usajili kwa kishindo.

Klabu ya Singida United inayodhaminiwa na kampuni ya kubashiri michezo ‘SportPesa’ yafunga usajili kwa kishindo na sasa ipo tayari kwa mikiki mikiki ya Ligi kuu Tanzania Bara.


Singida United ambayo inatarajia kushiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza imefanikiwa kumchukua nahodha wa timu ya APR ya Rwanda, Michel Rusheshangoga na beki  wa kulia wa timu ya taifa ya nchi hiyo.

Michael Rusheshangonga ambaye ametwaa tuzo ya goli bora la msimu kwa ligi kuu ya Rwanda ametua nchini na kwenda moja kwa moja kuungana na wenzake waliopo kambini Mwanza.
Mfungaji wa goli bora la msimu ligi kuu ya Rwanda, Michael Rusheshangonga

Katika kuhakikisha timu hiyo imejipanga kuleta ushindani na ikiwezekana kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu ujao, imemtambulisha rasmi mfungaji bora wa misimu miwili mfululizo ya ligi ya Rwanda, Dany Usengimana.
Mfungaji bora wa misimu miwili mfululizo ya ligi ya Rwanda, Dany Usengimana(kulia) akipeana mokono na Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga(kushoto)Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment