Tuesday 18 July 2017

VIDEO: Tundu Lissu Ataka Rais Magufuli Asusiwe Kila Mahali na Mataifa Mengine Duniani.

Mbunge wa Singida Mashariki amefanya mkutano na waandishi wa habari akimtuhumu Magufuli kwa mambo mengi na kutaka asusiwe kila mahali.

Amesema mataifa ya nje yanayompa hela Magufuli yamsusie Magufuli na kutompa pesa za kuikandamiza Tanzania. Kujenga uwanja wa ndege Chato ni kama Mobutu Seseseko alivyojenga kijijini kwao.

Amesema Mwinyi na wengine wanaotaka Magufuli aongoze miaka zaidi ya 10 wanataka Magufuli awe kama rafiki zake Nkurunziza, Kagame na Joseph Kabila na kuita huo ni ujinga. Wanaoshangilia Bombardier hawajui zimenunuliwaje na Magufuli anaendesha nchi kwa misingi ya kikabila na Kifamilia, akimtolea mfano Dotto James Katibu Mkuu wizara ya fedha na Naibu wake ni watoto wa dada alikuwa afisa ngazi za chini wa TANROADS miaka 2 iliyopita na wanaambiana mjomba tununue ndege, tujenge uwanja wa ndege nyumbani na hela zinatoka.

Mmoja wa wanasheria wa wizara mmoja Medad Kalemani na Naibu Waziri nishati na madini hakufukuzwa kwenye skendo ya madini iliyomuondoa Muhongo. Kuingilia uhuru wa mahakama. Anawaambia majaji kwenye mikutano ya hadhara namna ya kutoa hukumu.

Sasa ni mwezi wa 8 mahakama ya Tanzania haina Jaji mkuu ina Kaimu jaji mkuu na hii haijawahi kutokea Magufuli anajiona yeye ndio dola kwenye karne ya 21. Majaji wa mahakama kuu 4 kujiuzulu ndani ya miezi 3 haijawahi kutokea na sababu wala maelezo hayatolewi japo kuna baadhi yao walihusika na Escrow ila haijatolewa sababu

Kama majaji wanalazimishwa kujiuzulu bila maelezo nani yupo salama?
Vyombo vya habari vinavamiwa kwa bunduki na hakuna hatua inayochukuliwa
Tunaposema udikteta ndio huu. Kazi ya kupinga udikteta sio ya CHADEMA tu, ni vyombo vya habari, wafanyakazi wa serikali viongozi wa dini. Kutumia vibaya fedha na rasilimali za taifa.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment