Monday 17 July 2017

MBUNGE Goodluck Mlinga Azidi Kutetea Diamond Kuchongewa Sanamu la Heshima Aliyoipa Tanzania.

Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Mh #GoodluckMlinga amezidi kutetea hoja yake ya kuwa wasanii waliofanya vizuri na kuiwakilisha nchi nje vizuri, kupewa heshima kama kujengewa sanamu na baadhi ya mitaa na barabara kupewa majina yao.
.
.
Kipindi cha nyuma Mbunge huyo alisimama Bungeni na kusema kwa namna msanii #DiamondPlatnumz anavyoiwakilisha nchi vizuri kimataifa anastahili kujengewa sanamu, na kupendekeza ikibidi sanamu la askari posta Dar es Salaam liondolewe na kuweka hilo la #Diamond.
.
.
#GoodLuck👉“Na sikumtaja Diamond pekee, niliwataja wasanii wengi kama wakina Mr Nice ambao wameiwakilisha Tanzania sana nje lakini mpaka leo hii wamepotea hawana alama, inakuwa hawawezi kuwahamasisha wasanii wengine, lakini tunapoweka alama kila msanii anapofanya vizuri tunahamasisha wengine na ndiyo utaratibu katika nchi za wenzetu,” ameiambia Habari Xtra ya Times Fm
.
.
Na kuongeza👉“Kuna mchezaji mmoja wa mpira alitoka Kenya (Victor Wanyama) kuja Tanzania siku ya pili alipewa mtaa, sasa vile vitu ndio tunatakiwa tuvifanye kwa wasanii wetu wanaoibeba nchi. Sasa wewe fikiri mtu katoka nje ambaye anawakilisha nchi nyingine tunampa mtaa, lakini kwetu ni msanii gani alishawahi kuacha alama hata akapewa Barabara, hakuna!!!,” .
.
.
JE UNAMUUNGA MKONO MBUNGE HUYU AU UNAMPINGA??

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment