Sunday 23 July 2017

SHABIKI WA MAN UNITED AMVAA ROONEY BAADA YA KUREJEA ENGLAND, APIGA NAYE PICHA.

Hatimaye Wayne Rooney amerejea nchini England na kikosi kizima cha Everton baada ya mzunguko mrefu wa ziara za mechi za kirafiki kujiandaa na Ligi Kuu England.


Shabiki mmoja wa Man United alimvaa Rooney licha ya kuwepo kwa askari na kuomba kufiga naye picha kwa mtindo wa selfie.

Shabiki huyo aliyekuwa na jezi ya Man United alishindwa kujizuia na Rooney hakufanya ajizi, alishirikiana naye vizuri kabisa.

Everton ilianza ziara yake nje ya England kwa kucheza na Gor Mahia jijini Dar es Salaam, ikapaa hadi Uholanzi kabla ya kumalizia ziara hiyo Ubelgiji ambako ilicheza na timu ya Genk anayoichezea Mtanzania Mbwana Samatta.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment