Tuesday 11 July 2017

Picha: Gor Mahia watua Bongo kuwavaa Everton.

Mshindi wa SportPesa Super Cup 2017, Gor Mahia ya nchini Kenya imewasili nchini mchana huu kwaajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Everton.

Mchezo huyo utachezwa Alhamisi hii Julai 13 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Gor Mahia jioni ya leo watatembelea uwanja wa taifa kwaajili ya mazoezi ya mwisho.

Timu ya Everton inatarajiwa kuwasili nchini Jumatano hii huku ikiwa na mchezaji wake mpya, Wayne Rooney waliomsajili kutoka Manchester United.

Tayari homa ya mpambano huo miongoni mwa mashabiki nchini imeendelea kuwa kubwa huku wengi wakiwa na shauku ya kuwaonya nyota mbalimbali wa Everton kama vile Jordan Pickford, Ross Barkley, Idrissa Gana Gueye na wengine wengi.

Viingilio vya mchezo huo ni Sh 8000/= kwa VIP C na Sh 3000/= kwa viti vya mzunguko na mchezo unatarajiwa kuanza majira ya saa 11 jioni. Angalia picha.
 Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment