Monday 19 February 2018

Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) Mwakani Kupigwa Uwanja wa Uhuru.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametaja viwanja vitakavyotumika katika mashindano ya vijana chini ya miaka 17 katika fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani.

Waziri Mwakyembe alisema Uwanja wa Taifa utatumika kwaajili ya ufunguzi na kufungukia mashindano hayo, huku viwanja vingine vya Uhuru na Azam Complex Chamazi vikitumika katika mechi za mashindano hayo.

"Tunataka tufanye mabadiliko katika hizi nyasi bandia za uhuru tuweke mpya, lakini uwanja wa Gymkhana utatumika kwa mazoezi, bado kuna viwanja vingine tunaendelea kuvichagua ili timu zipate sehemu ya kufanyia mazoezi kwa urahisi," alisema Mwakyembe.

Waziri Mwakyembe alisema wanajua wingi wa timu nane zinazokuja zitakuwa na viongozi, wachezaji na mashabiki hivyo wanajiandaa kuhakikisha wageni hao wanapata mahitaji yao mapema.

"Magari yanahitajika kwaajili ya kuwabeba wageni wetu hivyo inabidi yapatikane na kuandaliwa mapema, lakini pia tunajupanga juu ya suala la foleni wasiweze kukutana nalo,'' alisema.

Mwakyembe aliongeza kwamba wanaendelea na maandalizi, wapo katika hatua nzuri kwa ajili ya mashindano hayo. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment