Wednesday 21 February 2018

Vanessa Mdee Afata Nyayo za Alikiba, Ommy Dimpoz na Ben Pol Naye Abadirisha Rangi ya Nywele.

Ben Pol ameonekana kuwavutia wasanii wa Bongo Flava kwa mwaka huu katika staili ya kuweka rangi nywele (breach). Baada ya Alikiba na Ommy Dimpoz kufanya hivyo, Vanessa Mdee ameamua kufuata nyayo hizo.

Vanessa amepost picha tatu katika mtandao wake wa Instagram ambazo zinamuonyesha akiwa katika muonekano wake mpya wa nywele zikiwa na rangi ya karoti.

New Hair Who Dis? @iambenpol najua umefarijika sana 🤣📸 ,” ameandika Vee kwenye moja ya picha alizoziweka kwenye mtandao huo.

Naye Ben Pol amemjibu Vanessa kupitia mtandao huo kwa kuandika, “Happy Faraja Week, naendelea kufarijika tu 😀 @vanessamdee 😍🧡.”

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment