Sunday 4 February 2018

Mke wa Mzee Majuto: Namuombea Sana Mume Wangu Apone Maana Ndiye Furaha Yangu.

MKE wa mchekeshaji maarufu Bongo, Amri Athuman ‘Majuto’, Aisha Yusuf amesema kuwa siku za hivi karibuni alipoanza kuugua tena mumewe amekuwa akikesha na kumuombea arudi katika hali ya kawaida kwani anapoumwa vitu vyote vinalala.

Akichonga na gazeti hili mke huyo alisema mume wake ni mcheshi sana na ni mtu anayeifanya familia kuwa na furaha kila wakati sasa anapokuwa mgonjwa nyumba inakuwa haina amani kabisa na hata watoto ambao amezoea kucheza nao wanapoa.

“Kila siku dua zangu ni kwa mume wangu maana ndiyo nguzo katika familia yetu na ni mtu mcheshi sana kwa familia hivyo namuombea sana apone maana ndiye furaha yangu,“ alisema mke wa Majuto.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment