Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>Kubenea afunguka baada ya Serikali kulifungia gazeti la Mseto.Fahamu zaidi hapa.
Siku moja baada ya Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni,
Michezo na Sanaa kutangaza kulifungia gazeti la Mseto kwa kipindi cha
miaka mitatu, Mbunge wa Ubungo ambaye pia ni mmoja wa Wakurugenzi wa
Kampuni ya Hali Halisi inayotoa gazeti hilo, Saed Kubenea amenena.
Jana, Waziri Nape Nnauye alieleza kuwa wameamua kulifungia gazeti
hilo kutokana na kuandika habari za uongo, kutumia nyaraka za kugushi
pamoja na kumchafua Rais John Magufuli pamoja na Serikali kwa ujumla.
Hata hivyo, Kubenea ameeleza kupingana na uamuzi wa kulifungia gazeti
hilo akidai kuwa ni mkakati ulioandaliwa dhidi ya vyombo vya habari
nchini kwani hata hoja zilizotolewa wao hawakupewa nafasi ya kuzijibu.
“Hatukusikilizwa kutokana na hoja tuliyotakiwa kujibu ikiwemo ya
kumchafua Rais Magufuli, huu ni mkakati kwa vyombo vya habari nchini,”
Kubenea aliiambia Mtanzania.
Kubenea alieleza kushangazwa na kauli ya Serikali kuwa gazeti hilo limekuwa likionywa tangu mwaka 2012.
Mwanasiasa huyo machachari alisema kuwa Bodi ya Wakurugenzi wa Hali
Halisi itakaa Jumapili hii na kuamua hatua watakazochukua dhidi ya
uamuzi wa kufungiwa gazeti la Mseto.
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>Taarifa ya Ofisi ya Spika kuthibitisha kupokea hoja ya kumeondoa madarakani Naibu Spika.Fahamu zaidi hapa.
Ofisi
ya Spika imepokea taarifa ya kusudio la kuleta Bungeni Hoja ya
kumwondoa madarakani Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) iliyowasilishwa na Mbunge wa
Simanjiro Mhe. … Read More
#YALIYOJIRI>>>>Polisi Jijini Mwanza Wapambana na Majambazi kwa Saa 16,Wakamata Silaha Nzito, Watatu Wauawa.Fahamu zaidi hapa.
Watu
watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi,wameuawa katika majibizano ya
risasi na askari polisi mkoani Mwanza,alfajiri ya kuamkia jana jumapili katika mapango ya mlima wa Utemini yaliyopo kata ya Mkolani jijini Mwanz… Read More
#YALIYOJIRI>>>>MBWANA SAMATTA PAMOJA NA WASANII WA SHIWATA WAKABIDHIWA MAENEO YAO KATIKA KIJIJI CHA WASANII WILAYANI MKURANGA..FAHAMU ZAIDI HAPA.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Bi. Leah Kihimbi (katikati) akimkabidhi cheti cha umiliki wa
eneo la ukubwa wa ekari tano baba yake Mbwana Samatta kwa niaba ya
mwanae Mb… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Bunge Kuzungumzia Sakata la Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.Fahamu zaidi hapa.
KATIBU
wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah leo ataeleza kinachoendelea kuhusu
kusudio la Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kutaka kumwondoa madarakani
Naibu Spika, Dk Tulia Ackson (pichani).Kambi hiyo inayoongozwa
na Mwenyeki… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Msanii Diamond Atoa Msaada Wa Madawati 600 Kwa Mkuu Wa Mkoa Wa Dar Es Salaam Mhe. Makonda.Fahamu zaidi hapa.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akimpongeza Mkurugenzi wa
WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' mara baada ya kumtembelea
ofisini kwake na kutoa mchango wake wa madawati yapatayo 600 kwa ajil… Read More
0 comments:
Post a Comment