Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop, Dudu Baya amedai ukimya wake kwenye
muziki umesababishwa na kuwa busy kwenye biashara na siyo kwamba
amefulia kama baadhi ya watu wanavyodai.
Rapper huyo amedai kwa sasa maisha yake yako Mwanza na Kampala akija Dar
anakuja kufanya kazi za kisanaa japo alishaamua kupotezea muziki na
kufanya biashara zake mbalimbali kwa kuwa haishi kwa kutegemea mziki
pekee.
“Dudu Baya sijafulia kama watu wanavyodhani mimi na biashara zangu
nyingine na muda mwingi sipo Dar es Salaam. Watanzania ndiyo tabia yao
hiyo wakiona msanii haonekani wanadhani amefulia mfano watu walipoona
King Crazy GK amepotea walidhani amefulia kumbe alikuwa chimbo anapiga
kitabu na saizi tayari ana masters yake” Dudu Baya alikiambia kipindi
cha Planet Bongo cha EA Radio.
Pia Dudu amesema kauli ya Darasa kuimba kwamba ‘siyo chui, simba wala
mamba ngozi yake inamtosha kujigamba’ haijamsumbua kwa kuwa Darasa ni
kijana wake na ni msanii ambaye amepambana kwa muda mrefu ila kwa sasa
kafanikiwa hivyo anampongeza kwa mafanikio
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment