Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein
akikagua gwaride la vikosi mbalimbali vya kijeshi katika sherehe za
mapinduzi, miaka iliyopita
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed
Shein, leo anatarajiwa kuwaongoza maelfu ya Wazanzibar na Watanzania kwa
ujumla katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Sherehe za maadhimisho hayo ambazo mwaka huu zimeanza mapema zinafikia
kilele hii leo katika uwanja wa amani visiwani humo huku ukitarajiwa
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali za pande zote mbili,
mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa.
Pamoja na mambo mengi uwanjani hapo Rais Shein anatarajiwa kukagua
gwaride maalum lilioandaliwa kwa ajili ya maadhimisho hayo ya mapinduzi
matukufu katika visiwa hivyo.
Kwa upande wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John
Magufuli, yeye ataongoza wananchi wa Tanzania Bara katika maadhimisho
hayo akiwa mjini Shinyanga kwa mkutano mkubwa wa hadhara unaofanyika
katika uwanja wa Kambarage.
Mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika Januari 12 mwaka 1964, yakiongozwa na Rais wa Kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Aman Karume.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment