Serikali
ya Jamhuri ya Muungano Tanzania, imeanzisha rasmi vita kwa wanamichezo
na viongozi wa michezo mbalimbali ambao wamekuwa wakihusika na dawa za
kuongeza nguvu michezoni.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa tume ya taifa ya Shirika la Umoja
wa Mataifa la Elimu, Sanaa na Utamaduni (Unesco), Dk. Moshi Kimizi
katika semina ya siku moja ya udhibiti wa dawa hizo.
Kimizi
alisema Tanzania imesaini mkataba maalum na Chama cha Kuzuia Dawa
Haramu Michezoni Duniani (Wada), hivyo ina wajibu wa kuhakikisha
wanamichezo wake wanajihepusha nazo ili kuficha aibu ya taifa.
“Semina
hii ya siku moja itasaidia kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wa michezo
katika kusaidia upigaji vita matumizi ya dawa za kuongeza nguvu
michezoni ambazo zinasababisha matokeo yasiyo halali.
“Kwa
kushirikiana na wizara husika ya michezo, tunaamini tutafanikiwa kupiga
vita dawa hizo na hatutoweza kuvumilia kuona vipaji vya wachezaji wetu
vinapotea kwa sababu ya madawa ya kuongeza nguvu michezoni.
“Na
hii itasaidia kuficha heshima ya taifa, chama husika na mchezaji pale
itapogundulika mchezaji anatumia dawa hizo mara baada ya kushinda
mashindano atakayoshindana,” alisema Kimizi.
Mkufunzi
katika semina hiyo, Dk. Henry Tandau alisema kuwa vita dhidi ya
matumizi ya dawa hizo, siyo nyepesi na inahitaji nguvu za pamoja
kukomesha.
“Matumizi
ya dawa hizi ni biashara kubwa ambayo mtu mmoja au watu wachache
hawawezi kuidhibiti. Ni vigumu kwa mtu wa kawaida kufanya hivyo kwani
hufanyikia kwenye maabara ambazo humilikiwa na watu wenye uwezo mkubwa
wa kifedha,” alisema Tandau.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment