CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo kinafanya vikao viwili vikubwa kwa mkupuo
vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini hapa.
Vikao hivyo vitafanyika kwa siku moja, baada ya Kamati Kuu kutofanyika
jana. Badala yake siku nzima ya jana, ilitumika kwa ajili ya kikao cha
Kamati ya Usalama na Maadili ya chama.
Kikao hicho cha Kamati ya Usalama na Maadili cha jana, kiliangalia
maadili ya wanachama wake na kiliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM,
Rais John Magufuli.
Pamoja na mambo mengine, kikao hicho hujadili nidhamu za viongozi na
baadhi ya wanachama waliokwenda kinyume na maadili ya chama hicho.
Kamati hiyo huhoji wanachama na viongozi na mapendekezo yake, hupelekekwa Kamati Kuu kwa ajili ya hatua zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi, Humphrey Polepole alisema, vikao hivyo vitafanyika leo, ambapo
Kamati Kuu itakutana asubuhi.
Alisema baada ya Kamati Kuu kumaliza kikao chake, mchana Halmashauri Kuu
itafanya mkutano wake, ambao ndio utakaoandaa ajenda kwa ajili ya
Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho, utakaofanyika kesho, ambao utafanya
mageuzi makubwa katika chama.
Baadhi ya mageuzi hayo ni kubadilisha Katiba na Kanuni za chama pamoja
na jumuiya zake, ikiwemo kupunguza wajumbe wake ili kuwa chama cha
ufanisi zaidi.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment