STRAIKA wa Zanaco ya Zambia, Kwame Attrams, raia wa Ghana, amesema anatamani siku moja kuja kukipiga Simba.
Attrams ndiye aliyeisawazishia Zanaco baada ya Yanga kutangulia kufunga
wakati walipotoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa Ligi ya
Mabingwa Afrika uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na juzi, Attrams alisema akizichezea Simba inaweza kuwa njia ya kwenda kusakata kabumbu Ulaya.
Attrams alisema lakini atakuwa tayari kuichezea Simba kwa kuwa ni timu
kongwe na zinafuatiliwa na mashabiki wengi barani Afrika ikiwamo nchini
Ghana.
Straika huyo aliyezichezea timu za Groupe Spotive Bazano ya Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo na Wadi Degla ya Misri, alisema malengo yake ni
kutaka kuona siku moja anacheza soka Tanzania katika klabu hizo mbili
zenye historia kubwa.
“Simba na Yanga ni timu kubwa, nimeanza kuzisikia tangu nikiwa mdogo
natamani siku moja na mimi nije Tanzania kufanya kazi na moja ya klabu
hizi,” alisema Attrams.
Alisema anajisikia furaha kuifunga Yanga kwa kuwa ni timu kubwa na
tayari ameingia katika historia ya kuwatungua Wanajangwani hao.
Attrams alisema atajisikia zaidi akicheza pamoja na Waghana wenzake wanaokipiga Simba, James Kotei na Daniel Agyei.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment