Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dr Jakaya Kikwete anazindua taasisi yake
muda huu. Miongoni mwa timu ya taasisi hiyo ni Prof Mahalu ambae ni
daktari bingwa wa moyo, Mkandara na Ombeni Sefue huku Kikwete akiwa
mwenyekiti wa taasisi. Bodi ya taasisi hiyo pia imejumuisha wajumbe
wengi kutoka nje ya nchi.
Hii inakuwa taasisi ya tatu inayoanzishwa na kubebwa na majina ya marais
wastaafu ikitanguliwa na taasisi za Mwl Nyerere(Mwl Nyerere Foundation)
na Mkapa Foundation huku Mwinyi yeye akipita kimya kimya.
Kulingana na taasisi hiyo, itajihusisha na afya hasa ya mama na mtoto,
kudhibiti Maleria na lishe bora. Pamoja na hayo taasisi hiyo
itajihusisha na elimu hasa ya vijana, kukuza vipaji, ujasiriamali na
mafunzo. Mratibu wa taasisi hiyo, Omary Issa ambaye aliteuliwa na JK
wakati wa utawala wake kuongoza 'Matokeo makubwa sasa' amesema Kikwete
ameamu kutoa utaalamu na maarifa yake kwa watanzania na waafrika kwa
ujumla.
Wengine katika taasisi hiyo ni Jack Steve ambae ameshawahi kuwa balozi
wa Marekani nchini Tanzania, Aboubakar Bakhresa ambae ni mfanyabiashara,
Indriss Jala ambae ni waziri katika serikali ya Malaysia, Kisangugi
ambae ni mmarekani mwenye asili ya Tanzania na mfanyibiashara.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment