Ikiwa sasa ni takriban miaka miwili tangu aliyekuwa Mkurugenzi wa
Tanzania One Theatre (TOT), Kampteni John Komba, kufariki Dunia, Mtoto
wake Gerald John Komba, ameibuka na kutoa wimbo wa kuiunga mkono
Serikali katika mapambano yake mapya dhidi ya dawa za kulenya nchini
Tanzania.
Gerald aliyezaliwa mwaka 1986 jijini Dar es salaam, amesema, ameamua
kutoa wimbo huo wenye maudhi ya kwaya, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya
kifo cha Baba yake, Marehemu John Komba aliyefariki Dunia, Februari 28,
2015 katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar e Salaam,
alikopelekwa baada ya kuzidiwa ghafla akiwa nyumbani kwake, Tangibovu
kwa Komba.
Mtoto huyo wa Jihn Komba aliyekuwa mwanamuziki nguri wa utunzi na
uimbaji wa nyimbo za kwaya, amesema, wimbo aliotoa nimarejeo ya wimbo
ambao ulitungwa na nguri huyo, kukemea usambazaji na matumizi ya dawa za
kulevya miaka zaidi ya kumi iliyopita, lakini baada ya kuurekodi
haukuwahi kuimbwa na TOT wala kuchezwa kwenye vituo vya Radio au
Televisheni.
Gerald ambaye amesomea Sheria katika Chuo Kikuu cha Saint Augustine
kilichopo Mwanza, Tanzania, baada ya masomo ya shule ya Msingi katika
shule ya Kawe “A” na shule yasekondari Mbezi Beach High school, anasema
katika kuutoa wimbo huo, hakubabaisha kwa kuwa na yeye anacho kipaji cha
kuimba japo amekuwa hakitumii sana. Zamani Shule ya Kawe A’ ilifahamika
kwa jina la Tanganyika Packers, lakini baada ya aliyekuwa Rais wa Awamu
ya Pili, Ali Hassan Mwinyi kubaini kuwa kiwanda cha kusindika nyama cha
Tanganyika Packers kimeshakufa, akaamua shule hiyo kubadilishwa jina.
“Nimeanza kupenda sanaa ya muziki tangu nilipokuwa mtoto, kwa kuwa
nilikuwa naenda na Baba (John Komba) kwenye maonesho yake na kundi la
TOT, na nilikuwa navutiwa sana na namna baba yangu alivyokuwa akitamba
jukwaani wakati akiimba”, alisema Gerald.
“Tangu wakati huo, nilikuwa napenda kukariri nyimbo zote za Baba, na
hakuna wimbo nisioujua kuanzia ala hadi mpangilio wa mashairi, lakini
pia pia shuleni nilikuwa naimba kwenye kwaya ya shule, na siku za
karibuni nimekuwa pia nikiimba kwaya kwenye Kanisa la Praise team, hapa
jijini Dar es Salaam”, aliongeza.
Anasema, ameambua kuurudia wimbo wa Marehemu Baba yake kwa sababu,
kwanza yeye binafsi anachukia mamia ya vijana wanavyoharibika kwa
matumizi ya dawa za kulevya kwa namna ambavyo wanatumiaji wengi wa dawa
hizo hukatishwa ndoto zao mbalimbali za kuwa watu muhimu katika ujenzi
wa taifa la Tanzania.
“Kwanza ukizingatia hakuna aliyezaliwa teja, wengi wanaokuwa hivyo
wanakutana na hili balaa wanapoingia kwenye jamii kwa hiyo nikaona
nifanye kitu ili jamii iweze kutoa mchangu wangu katika kuelimisha
jamisha jamii ili izinduke na kuelewa namna dawa hizi za kulevya zilivyo
za hatari.
Pili niliamua kuurudia wimbo huu kwa sababu, watu wengine hasa Walimu na
Wazazi wengi wao wanajisahau katika kusimamia malezi ya vijana. Wazazi
wanamwachia Mwalimu jukumu la kutazama mwanafunzi akiwa shule bila kujua
mtoto anaharibika katikati ya shule na nyumbani wakati wa kwenda na
kurudi nyumbani, kwa hiyo Mwalimu na mzazi ni Watu muhimu wa kuchunga
mwanafunzi”, alisema Gerald.
Anasema, sababu yake ya tatu ya kuamua kuurudia na kuongeza vionjo
kwenye wimbo huo ni kusisitiza kuwa mapambano hayo ni ya Watanzania wote
ambapo anasema ameweka baadhi ya majina ya wakuu wa mikoa kwenye wimbo
huo kwa kuwa vita hii ya mapambano dhi ya dawa za kulevya ni ya
Watanzania wote na hao ndiyo wawakilishi wa Rais kwenye kila mkoa.
“Nimeongeza vionjo kwa kutaja hawa wakuu wa mikoa kwa kuwa najua hawa
ndiyo waakilishi wa Rais, na Rais Dk. John Magufuli hawezi kukabiliana
nayo peke yake hivyo unahitajika ushirikiano na wananchi kuanzia ngazi
ya Kaya, Vijiji, Kata, wilaya hadi mkoa.
Na mwisho niliamua kuurudia kama Kumbukumbu ya miaka miwili ya kifo cha
Marehemu Baba, ukiuusikiliza wimbo huu utangua kuwa sauti yangu na yake
zimefanana kwa karibu sana katika uimbaji, hivyo itaweza kuashiria kuwa
yale alyolenga kuyakemea kwenye nyimbo zake, hata baada ya kufariki
dunia lakini bado kuna mtu mwingine ambaye ni mtoto wake atakayeendelea
nyimbo hizo kufanya lengo lake la kuionya jamii ibaki pale pale”,
alisema Gerald
“Mtindo nilioutumia kwenye wimbo huu ni uleule wa kwaya aliotumia Baba,
na nimeuimba upya kwa kushirikiana na Mama yangu Mzazi, Jane Mkondwa
ambaye ni mwimbaji wa miaka mingi katika Kundi la TOT, Nimeurekodi
katika Studio za PM Records chini ya Mtayarishaji anayefahamika kwa jina
la Testimony.
“Baadhi ya maneno yaliyomo kwenye wimbo huu ni maneno ambayo ambayo
hutumiwa zaidi na mateja na nimefanya hivyo kwa kuwa ni miongoni mwa
walegwa katika vita hii. Hivyo, nikaona nitumie maneno wanayoweza
kuyaelewa haraka kama; ‘nywele misumari’, ‘twende kilioni’, ‘Macho
kufutuka’, ‘akili inayeya’ ambapo neno kama akili inayeya kwa teja
humaanisha anavyokuwa baada ya kulewa dawa za kulevya yaani ufahamu
katika akili zake unapotea.
“Maneno mengine ni Gheto na Washkaji (nyumba wanapoishi vijana wa kiume
au wa kike, lakini neno mshkaji au washkaji unategemea na umri, wale wa
miaka ya 1960 walimaanisha wanawake wao lakini wa sasa wanamaanisha
marafiki wao ingawa maana zote mbili zina maana sawa”, anafafanua
Gerald.
Anasema, kwa sasa wimbo huo bado upo katika sauti tu (Audi), kwa kuwa
hajapata uwezo wa kuurekodi katika video, ingawa yupo katika jitihada za
kutafuta uwezo ili kuhakikisha anaurekodi katika video ili ujumbe uweze
kufika kwa urahisikwa walengwa wote.
Gerald anatoa mwito kwa Watanzania kuungana ili tulitokomeza usambazaji
na matumizi ya dawa za kulevya bila kujali itikadi za vyama, kabila,
jinsia kwa kuwa ni janga linaloweza kuingia katika familia, Taasisi,
Chama cha siasa, kabila au jinsia yoyote.
“Watanzania wenzangu naomba kila atakayepata fursa ausikilize kwa makini
wimbo wangu huu, ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Dk. John
Magufuli katika mapambano haya mapaya dhidi ya usambazaji na matumizi ya
dawa za kulevya katika nchi yetu ya Tanzania”, anasema Geral
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment