Thursday 16 June 2016

Aslay na Ruby wasema kuwa hawana uhusiano, wadai ilikuwa kiki tu.Fahamu zaidi hapa.

Aslay na Ruby ameibuka kutolea ufafanuzi tetesi zilizoibuka za kuwa wana uhusiano wa kimapenzi.

Tetesi hizo zilianza baada ya wenyewe kuanza kupostiana na caption za utata zilizopelekea mashabiki kuamini wawili hao walikuwa couple mpya mjini.

“Unajua siku hizi maisha yamebadilika na mashabiki wanapenda sana kiki,” Ruby alifunguka kwenye kipindi cha Planet Bongo ya Eatv Radio.  “Hivyo kwa kuwa wanapenda hayo ilibidi tuwape kitu roho inapenda lakini ukweli ni kwamba mimi na Aslay ni marafiki tu si wapenzi kabisa, ilikuwa kiki tu hiyo ili kusaidia kazi hii kufika sehemu kwa haraka”

Kwa upande wake Aslay alipoulizwa juu ya suala hilo alisema kuwa kitu alichosema Rubby ndiyo uhalisia wenyewe na kukana si wapenzi kama ambavyo awali tetesi zilivyokuwa zikienea kwenye mitandao ambazo zilitengenezwa na wao wenyewe.

Ruby ameshirikishwa kwenye wimbo mpya wa Yamoto Band ‘Su’

Source: Eatv

0 comments:

Post a Comment