Kocha
Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface
Mkwasa, amefanya mabadiliko kwenye kikosi kinachotarajiwa kusafiri
Jumatano Agosti 31, 2016 kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa
kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017)
dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.
Mabadiliko
yaliyofanyika ni kwa kumchukua Kipa kinda wa JKT Ruvu, Said Kipao
kuchukua nafasi ya Deogratius Munishi ambaye amefiwa na baba yake mzazi
katika kifo kilichotokea jijini Dar es Salaam jana Agosti 28, 2016.
Kipao
alikuwa nyota wa mchezo katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba na
mechi ikaisha kwa sare ya bila bao huku yeye akionyesha umahiri mkubwa
wa kuokoa michomo ya washambuliaji na viungo wa Simba.
Licha
ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania
nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa
ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo
mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa
katikati ya mashindano.
Wachezaji wanaounda kikosi hicho kwa sasa na kuanza kuingia kambini Hoteli ya Urban Rose jijini Dar es Salaam ni:
Makipa-
Said Kipao – JKT Ruvu
Aishi Manula – Azam FC
Mabeki
Kelvin Yondani - Young Africans
Vicent Andrew - Young Africans
Mwinyi Haji - Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
Shomari Kapombe - Azam FC
David Mwantika - Azam FC
Viungo
Himid Mao - Azam FC
Shiza Kichuya – Simba SC
Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Juma Mahadhi - Young Africans
Farid Mussa Tenerif ya Hispania
Washambuliaji
Simon Msuva - Young Africans
Jamal Mnyate – Simba SC
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco - Azam FC
Mbwana Samatta - Genk ya Ubelgiji
0 comments:
Post a Comment