Saturday 27 August 2016

#MICHEZO>>>Thierry Henry Kuwa Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji Kuungana na Roberto Martinez.Fahamu zaidi hapa.

Kocha mpya wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez amesema mchezaji wa zamani wa klabu za Arsenal na Barcelona, Thierry, ambaye aling’aa sana wakati akichezea timu ya taifa ya Ufaransa, atakuwa mmoja wa wasaidizi wake.
Henry alikuwa mmoja wa wakufunzi wa timu ya vijana Arsenal lakini akajiuzulu Julai baada ya meneja Arsene Wenger kumwambia kwamba hawezi kufanya kazi hiyo akiwa bado anaendelea kuwa mchanganuzi wa soka kwenye runinga.

Wakati wa Euro 2016 Henry alikuwa akifanya kazi ya kuchambua soka katika vituo vya Sky Sports na pia alifanya kazi na BBC Sport.

Thierry Henry alikuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1998 nyumbani.

0 comments:

Post a Comment