Sunday 12 June 2016

#YALIYOJIRI>>>>KAULI YA PADRI BAADA YA KUSHIRIKI FUTARI MSIKITINI DAR (+Audio).Fahamu zaidi hapa.

Desemba 23, 2015 Kiongozi wa dhehebu la kiislamu la Shia Ithna-sheriya Tanzania Sheikh Hemedi Jalala kuhusu kutoa mkono wa heri ya Krismasi alinukuliwa akisema Lazima tutambue kuwa binadamu wote ni ndugu ambao tumetokana na kizazi cha Adam na Hawa, na hivyo hakuna sababu za kuuvunja undugu huo

hata katika imani waislamu na wakristo wana amini kuwa Mungu ni mmoja na ipo siku ya hesabu ipo, na hivyo kitendo cha kuonana katika imani moja ni moja ya sababu kubwa ya kushirikiano” Alisema

Katika kuendeleza hilo jana jioni Sheikh Jalala aliamua kuandaa futari ya pamoja katika msikiti wa Masjid Alghadiir uliopo Kigogo Dar es salaam na kuialika kamati ya AMANI ya mkoa huo,  Kamati inayojumuisha viongozi wa dini mbalimbali ndani ya mkoa wa huo, ambayo iko chini ya uongozi wa mwenyekiti wake Samahat Sheikh Alhady Mussa Salim (sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam).

Sala ya jamaa ilisaliwa Masjid Alghadiir, Sala hiyo iliongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Samahat Sheikh Alhadi Mussa, na baada ya hapo futari ikaliwa kwa pamoja ambapo Padri John Solomoni alitumia dakika mbili kuiambia Www.Hebronmalele.blogspot.com kuwa baada ya kupata mwaliko wa futari alijiandaa kwa kufunga siku nzima.. mengine kuhusu tukio hilo ameyasema yote kwenye sauti hapo chini baada kushiriki futari jana jioni.
Sheikh mkuu wa Dar es salaam Alhady Mussa Salim ambaye ni M/Kiti wa kamati hiyo(Kulia), Padri John Solomoni (Kushoto) ambaye pia ni katibu wa kamati hiyo.


0 comments:

Post a Comment