KATIBU MKUU WA TFF, MWESIGWA CELESTINE
Wiki
iliyopita Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro,
alitangaza kuendelea kupiga kazi kama kawaida na kwamba hatambui adhabu
yake ya kufungiwa mwaka mmoja aliyopewa na Kamati ya Maadili ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwani hajapewa barua ya hukumu yake,
hata hivyo TFF imemwambia asithubutu kwani kama ni barua ya adhabu
alishakabidhiwa.
Muro,
juzi Ijumaa kwenye vyombo vya habari alisema alikuwa likizo na si
kutumikia kifungo hicho alichopewa baada ya kukutwa na hatia ya
kupingana na maamuzi ya TFF pamoja na kutakiwa kulipa faini ya milioni
tatu.
Katibu
wa TFF, Selestine Mwesigwa, ameliambia amesema kuwa Muro anajua nini
kitamtokea iwapo atathubutu kufanya kazi kwa sasa kutokana na adhabu
inayomtaka kutojihusisha na soka mwaka mzima.
“Yeye
anaongea lakini hajatuletea tamko lake rasmi na ataongea hukohuko,
lakini kwetu tunatambua adhabu iko palepale,” alisema katibu huyo.
Alipoulizwa
iwapo Muro ataanza kazi itakuwaje, Mwesigwa alisema: “Siwezi kusemea
tuhuma za ‘kama’ lakini ieleweke iwapo ikitokea, nadhani anajua adhabu
yake na kwa kuwa halijatokea (kufanya kazi kama alivyotamba) tuliache
kwanza.”
Katibu
huyo wa zamani wa Yanga, alisema Muro alipewa barua ya hukumu ambayo
nakala yake ipo kwa waajiri wake, Klabu ya Yanga ambayo ilitumwa kwa
katibu, Baraka Deusdedit.
SOURCE: CHAMPIONI
0 comments:
Post a Comment