Simba imeuanza msimu vizuri kwa utambulisho wa kikosi chake kwa kufunga mabao matatu katika mechi moja.
Simba
imewatwanga wageni wake AFC Leopards ya Kenya kwa mabao 3-0 katika
mechi ya kirafiki maalum katika Simba Day iliyopigwa kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji
nyota wa Simba, Ibrahim Ajib aling’ara kwa kufunga mabao akianza na
dakika ya 38 kwa kushuti kali nje ya 18 kabla ya kuandika la pili katika
dakika ya 55.
Simba
ilikwenda mapumziko ikiwa na mabao mawili lakini kipindi cha pili,
mabadiliko yakaifanya kuwa bora zaidi na kufunga mabao mengine mawili
kupitia kwa Shiza Kichuya na Laudit Mavugo akafunga la nne katika
dakiaka ya 81.
Ivan Otieno, kipa wa AFC Leopards ndiye alikuwa kipingamizi kikubwa kwa Simba kufunga angalau mabao sita au saba.
Simba
inayofundishwa na Joseph Omog raia wa Cameroon, ndiyo ilishambulia kwa
kasi zaidi na kuwapa wakati mgumu Leopards waliokuwa wanaongozwa na
Raphael Kiongera.
PICHA ZA MATUKIO SIMBA DAY.
kikosi cha SIMBA FC
Kikosi cha AFC Leopards
0 comments:
Post a Comment