Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa vitendo wakati alipokagua maendeleo ya ukarabati na
upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma.
Imeelezwa
kuwa upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Dodoma utakamilika
mwishoni mwa mwezi Agosti ili kuruhusu ndege za abiria sabini mpaka
tisini kuweza kutua na kuruka na hivyo kurahisisha usafiri wa anga kwa
ukanda wa kati.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa baada ya kutembelea kiwanjani hapo kukagua hatua ya mwisho ya
ujenzi iliyofikiwa ambapo amesema kasi ya Mkandarasi Chicco
anayetekeleza kazi hiyo inaridhisha katika kuhakikisha kiwanja hicho
kinakamilika kwa muda na kwa viwango vilivyokubalika.
Amesema
mpaka sasa ni asilimia themanini ya kazi iliyotekelezwa kwa siku
arobaini na tano tangia kuanza ukarabati hivyo kasi iliyotumika kwenye
kiwanja hiki itatumika kwenye ujenzi wa viwanja vingine nchini.
"Tunaamini
kabisa kwa kasi ya mkandarasi na msimamizi mtakamilisha ujenzi huu
haraka na viwango tulivyokubaliana katika mkataba ili ndege kubwa zianze
kutua na kuruka" amesema Prof. Mbarawa.
Naye
Msimamizi wa ujenzi wa kiwanja hicho kutoka Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA) Eng. Mhandisi Mbila Mdemu amesema kazi ya ukarabati
na upanuzi inaendelea kufanywa usiku na mchana kwa kuzingatia ubora na
viwango na kukamilika kwa wakati
"Tulipewa
kazi hii na tunaahidi kuwa itakamilika kama tulivyoelekezwa ili kuwapa
wananchi wanaozunguka mikoa ya Dodoma na jirani fursa ya kutumia
usafiri wa Anga", amesema Eng. Mdemu.
Ameongeza
kuwa kazi zinazokamilishwa sasa ni kumalizia sehemu ya maegesho ya
ndege na tabaka la mwisho kwenye barabara ya kuruka na kutua ndege.
Mradi
wa upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Dodoma umegharamiwa
na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa zaidi ya shilingi
bilioni 11.8 na kukamilika kwake kutaongeza idadi ya safari za ndege
zitakazosafirisha abiria wa mikoa ya kanda ya kati.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa kutoka Eng. Guo Zhingjian wa kampuni ya Chicco inayojenga
kiwanja hicho Mkoani Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipokea taarifa ya maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma kutoka kwa Eng. Guo Zhingjian wa kampuni ya Chicco inayojenga kiwanja hicho, Mkoani Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipokea taarifa ya maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma kutoka kwa Eng. Guo Zhingjian wa kampuni ya Chicco inayojenga kiwanja hicho, Mkoani Dodoma.
0 comments:
Post a Comment