ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amesema hatua ya Rais John Magufuli kuzuia kufanyika kwa mikutano ya kisiasa nchini, imelenga kuminya demokrasia na serikali kutaka kutokosolewa.
Mgeja,
ambaye kwa sasa ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo
(Chadema), alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa hatua hiyo haikubaliki
katika nchi ya kidemokrasia duniani kwa kuwa uhai wa vyama vya siasa
upo katika mikutano.
Pia
amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi,
kushughulikia migogoro ya vyama badala ya kusubiri hadi nchi ikielekea
katika mgogoro mkubwa.
Alisema
kauli ya Rais Magufuli kwamba shughuli za kisiasa hadi mwaka 2020,
inakiuka katiba kwa kuwa mikutano na shughuli za vyama vya siasa vipo
kikatiba.
Alieleza kuwa kinachotokea sasa kwa viongozi wa upinzani ni kupigania demokrasia hali ambayo inaweza kuhatarisha amani ya nchi.
“Serikali
inakosolewa kupitia mikutano ya vyama vya siasa na serikali isitupangie
cha kuzungumza. Kutokana na kauli ya rais tunaonya likitokea lolote
katika mikutano ambayo itafanyika nchi nzima, kupitia operesheni ya
Umoja wa Kuondoa Udikteta Tanzania (Ukuta), Rais atawajibika iwapo nguvu
ya jeshi polisi itatumika,” alisema.
0 comments:
Post a Comment