Mbio
za Mwenge wa Uhuru zimetua Kanda ya ziwa huku zikizua sintofahamu kwa
watumishi wa umma waliotakiwa kutokukosa mkesha wake ili kukwepa rungu
la Mamlaka za kinidhamu dhidi yao.
Taarifa
kutoka wilayani Sengerema zilieleza kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya hiyo ameagiza watumishi wote wa wilaya hiyo kuhakikisha
wanahudhuria mkesha huo na kwamba daftari la mahudhurio litaitishwa
majira ya saa 6 usiku, saa 9 usiku na saaa 12 usiku.
Hayo yamebainishwa katika Tangazo rasmi lililosainiwa na Msangi M.A kwa niaba ya Mkurugenzi, Magessa Boniface.
Aidha,
katika Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, imeelezwa kuwa walimu wakuu
wa shule za msingi na sekondari waliitwa katika kikao na Mkuu wa Wilaya
hiyo, Mary Tesha ambaye aliwaeleza kuwa ambaye hatahudhuria mkesha huo
atakumbwa na adhabu ikiwa ni pamoja na kushushwa vyeo.
Hata
hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya alipotafutwa, alikana kuwaeleza walimu hao
kuwa wangeshushwa vyeo kama wasingehudhuria ingawa alikiri kuwa
alikutana nao.
“Sijasema
hayo, nilichosema ni kuwa Mwenge ni jukumu letu watumishi tunapaswa
kushiriki. Hao walimu ni wajumbe wa Kamati za Mbio za Mwenge hivyo
wanapaswa kushiriki. Hilo la kufukuza, kuwawajibisha hapana,” alisema Tesha.
Katibu
wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Nyamagana, Asha Juma
alisema kuwa ingawa amesikia kuwepo kwa maagizo hayo, hajapata
malalamiko kutoka kwa walimu.
“Najuwa wanahamasisha watumishi waende, lakini nadhani wangetafuta njia nyingine ya kuwahamasisha sio vitisho,” alisema Katibu huyo wa CWT.
0 comments:
Post a Comment