Serikali imesema ipo kwenye mchakato wa kuajiri walimu 4000 wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
Kauli
hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
wakati akiwa katika ziara yake ya kutembela wilaya mpya za jiji hilo,
akianzia na Kigamboni siku ya leo.
Majaliwa
amesema mchakato wa ajira hizo unaendelea chini ya Ofisi ya Rais
Utumishi, na muda wowote kutoka sasa mchakato huo utakapokamilika,
majina yatatolewa na walimu hao kuajiriwa.
Kuhusu
walimu wa masomo mengine, Waziri Mkuu amesema walimu wa masomo mengine
hususani ya sanaa wapo wa kutosha na kwamba wanapaswa kusubiri kwakuwa
wao wako wengi zaidi na hakuna uhaba na uhitaji wa walimu hao wa masomo
ya sanaa.
Hivi
karibuni, Wizara ya Elimu iliwataka wahitimu wa ualimu katika masomo ya
sayansi na hisabati kutuma taarifa (CV) zao ili izihakiki kabla ya
ajira, mchakato ambao tayari umekamilika na majina yalitumwa katika
wizara ya utumishi.
Naibu
Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella Manyanya wiki mbili zilizopita wakati
akiongea na kituo cha EATV alisema kuwa kazi ya wizara yake ilikuwa ni
kuhakiki taarifa za wahitimu hao, na si kuajiri, huku akibainisha kuwa
zoezi hilo limekamilika na majina yako utumishi ambao ndiyo watahusika
na kuajiri.
Pia
alisisitiza kuwa kama wizara ya elimu waliomba kupewa walimu wa masomo
ya Sayansi na Hisabati haraka kwa kuwa uhitaji wao ni mkubwa zaidi na
kuwataka wahitimu wote waliotuma taarifa zao, wasubiri watapata majibu
muda si mrefu.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment