Chama cha ACT-Wazalendo, kimemjibu Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM,
Hamphrey Polepole kwa kumueleza kuwa kazi chama cha siasa ni kuhangaika
na matatizo ya wananchi.
Juzi, Polepole aliwataka wapinzania kuacha kutumia matatizo ya
wananchi kujinufaisha kisiasa huku akitolea sakata la njaa na tetemeko
la ardhi liliotokea Bukoba.
Akizungumza na wanahabari jana (Jumatano) katika Makao Makuu ya
ACT-Wazalendo, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma kwa
chama hicho, Ado Shaibu amesema kukabiliana na matatizo ya wananchi
ndiyo mtaji sahihi wa kisiasa.
“Chama cha siasa lazima kishughulike na matatizo ya wananchi,
kisichojishughulisha na matatizo ya wananchi kitakufa,”amesema Shaibu.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment