BUNGE la Israel limeridhia muswada wa kwanza wa sheria, ambayo itaweka
kikomo cha adhana – wito kwa Waislamu kwenda misikitini kutekeleza ibada
ya sala.
Aidha unapiga marufuku matumizi ya vipaza sauti wakati wowote.
Hata hivyo, muswada wa sheria hiyo ulisababisha hasira kubwa miongoni mwa wabunge kutoka jamii ya Waarabu nchini hapa.
Muswada wa kwanza wa sheria hiyo unataka marufuku kwa mwadhini kutumia
kipaza sauti kati ya saa tano usiku na saa moja asubuhi, ukilenga adhana
kwa sala ya Alfajiri.
Mbali na muswada huo, mwingine unapendekeza marufuku kwa mwadhini
kutumia kipaza sauti katika mitaa yenye makazi ya watu, na faini ya
kiasi cha euro 2,600 itatozwa kwa yeyote atakayekiuka sheria hiyo.
Sheria ya kwanza itahusu misikiti katika eneo la Jerusalem Mashariki
linalokaliwa na Israel na pia maeneo yote ya nchi hiyo, lakini haigusi
viwanja vinavyouzunguka msikiti wa al-Aqsa ambavyo vimo katika mgogoro
huo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment