Wednesday 15 June 2016

Picha: Mke wa H. Baba, Flora Mvungi anatarajia kujifungua mtoto wa tatu.

Mke wa msanii wa muziki H. Baba, Flora Mvungi anatarajia kujifungua hivi karibuni na kuipatia familia yake mtoto wa tatu.

Flora Mvungi akiwa hospitali Wana ndoa hao wenye watoto wawili, Tanzanite na Africa, wameshare picha katika mitandao ya kijamii zenye ujumbe kuhusu ugeni huo.

Kupitia instagram, H.Baba aliandika.
Asante mungu kwa kila jambo #watoto nifaraja nakuombea muda ukifika ujifungue salama nakupenda mke wangu (1)tanzaniteone (2)Africa (???????) . Nitafutie jina la mwanangu Wa (3) nimuite nani.
Kwa upande wa Flora Mvungi, aliandika
Hahahhahahahahhahaah nacheka kwa raha yaani nafuraha sana mana naona watu maneno yanawatoka kila kona..kwani kuzaa ni kosa?au kuna siku nimemuomba mtu hela ya kutunza wanangu??waja mna tabu sana,jamani hebu tusipangiane jinsi ya kuishi,,kingine siko nje ya ndoa na hata ingekuwa nje ya ndoa pia ni watoto wangu..mwakereka na nini??. Hhahaaaaaa yaani mtasema sana..
Flora Mvungi akiwa na watoto wake
Tanzanite na Africa

0 comments:

Post a Comment