Mwishoni
mwa mwaka 2016, raia na wafuasi wa vyama vya upinzani nchini Zimbabwe
waliandamana kupinga utawala wa Rais Robert Mugabe ambaye amekuwa
madarakani tangu 1980.
Habari
zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya kimataifa zimedai kuwa maafisa
wa polisi nchini Zimbabwe wamemkamata mhubiri aliyetabiri kwamba Rais
Robert Mugabe atafariki mwezi Oktoba mwaka huu.
Pastor
Patrick Mugadza alikamatwa akiwa mahakamani mjini Harare Jumatatu
ambapo alikuwa ameenda kwa kesi nyingine dhidi yake. Wakili wake Gift
Mtisi amewambia waandishi wa habari kuwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka
ya kuvalia bendera ya taifa
Wakili wake ameimbia AFP kuwa; "Alikuwa
amefika mahakamani kwa kesi hiyo polisi walipomkamata wakati wa
mapumziko na kumfungulia mashtaka kwa sababu ya unabii huo"
Awali
alishtakiwa kwa kukosea heshima mamlaka ya Rais lakini shtaka hilo
likabadilishwa baadaye na kuwa amewatusi watu wa asili fulani au dini
fulani.
Pastor Mugadza wiki iliyopita aliandaa kikao na wanahabari ambapo alitabiri kwamba Mugabe atafariki Oktober 17 mwaka huu.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment