DAR ES SALAAM: Video queen matata ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha redio moja jijini hapa, Gift Stanford ‘Gigy Money’,
ametema cheche akisema kuwa, watu wote wanaomsema kwamba kutokana na
kuvaa nusu utupu na kujiachia na midume mbalimbali huenda ana maambukizi
ya virusi vya Ukimwi, waache kwani kama ni kweli basi wengi wangekufa
kwa sababu ameshatembea na mastaa kibao Bongo.
Akizungumza , Gigy alisema kwamba amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa mbalimbali wakubwa Bongo akiwemo Mbongo Fleva, Ali Kiba na kudai kuwa, kama kuambukizwa virusi angeanza yeye na wengine wangefuata.
“Unajua watu wanashangaza sana. Kama mtu
ana virusi vya Ukimwi hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu
anayempenda, ningependa watu waache unyanyapaa. Ninachojua mimi sina
Ukimwi kwa kuwa nilipima kwa shinikizo la mpenzi wangu wa sasa (Moulad
Alpha ‘Moj’) na watu niliotembea nao wanaendelea vizuri tu, wengine
wachumba zao wananyonyesha,” alisema Gigy.
Video queen huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, kuvaa nusu
utupu ni kitu anachopenda kufanya toka ndani ya moyo wake hivyo hakuna
mtu wa kumwambia kitu au kumkataza hata siku moja na wala siyo mgonjwa
wa akili bali anafanya kitu kujifurahisha nafsi yake si ya mtu mwingine.
“Mimi nasikilizaga moyo wangu unasema nini, si mtu anasema nini juu yangu hivyo kama kuvaa nusu uchi wana hofu na mimi waondoe hilo kwa maana kama ni Ukimwi wengi wangeondoka siku nyingi kwenye ramani ya dunia hii maana hakuna niliyemuacha kwa mastaa unaowajua,” alisema Gigy kwa kujiamini.
Gigy ameshatoka kwenye magazeti mbalimbali akidaiwa kutembea na mastaa kama Hemed Suleiman ‘PHD’, Richard Martin Lusinde ‘Rich Mavoko’, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Seif Shaban ‘Matonya’ na Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
Mwingine aliyewahi kutajwa ni Mtangazaji Gardner G. Habash ‘Captain’ na Mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment