Monday 27 March 2017

Mwakyembe Ameliagiza Jeshi la Polisi Kumuachia Huru Msanii Ney wa Mitego.Fahamu zaidi hapa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego.

Waziri ameishauri BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo huo, na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.

Dkt. Mwakyembe amesema kuwa hata Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO na kumshauri msanii huyo auboreshe wimbo wake kwa kutaja watu wengine kama wakwepa kodi, wauza unga, wezi pamoja na watu wengine wasio na maadili.

Aidha Baraza la Sanaa Nchini(BASATA) lilitangaza kuufungia wimbo huo na kutoa onyo kwa wote wanaosambaza wimbo huo mitandaoni.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment