Monday 27 March 2017

Ukweli Mchungu Kuhusu FARU John, Kamati Yabaini ni Kweli Alikufa.Fahamu zaidi hapa.

Kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuchunguza kifo cha Faru John imetoa taarifa kuwa mnyama huyo alikufa katika hifadhi ya Sasakwa Gruneti kwa kukosa matibabu alipoumwa.

Akiwasilisha ripoti hiyo kwa Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Samwel Mnyele alisema faru John alikosa matunzo na uangalizi wa karibu.

Mnyele ambaye ni Mkemia Mkuu wa Serikali alisema hakukuwa na kibali rasmi cha kumhamisha Faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Grunet.

Alisema kamati hiyo imeshauri hatua za kiutawala zichukuliwe dhidi ya ofisi ya Mkurugenzi wa Wanyamapori na Mhifadhi wa Hifadhi ya Ngorongoro kutokana na mapungufu yaliyojitokeza.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipongeza kamati hiyo na kusema serikali itayafanyia kazi mapendekezo ili kulinda maliasili.

Chanzo: Mwananchi

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment