Thursday 30 March 2017

Wakili kaeleza sababu za Mbunge Lijualikali kuachiwa huru.

Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam March 30 2017  imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya Kilombero dhidi ya Mbunge Peter Lijualikali baada ya kukubali kuwa hati ya mashtaka iliyomtia hatiani ilikuwa na mapungufu.

Mmoja wa mawakili waliokuwa wakisimamia rufaa ya mbunge Lijualikali, Fred Kiwelo amesema sababu mojawapo iliyopelekea kuachiwa huru ni pamoja na hati mashtaka kuwa na mapungufu ambapo kosa ambalo alikuwa amehukumiwa nalo limetofautiana na maelezo ambayo amesomewa.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment