Friday 31 March 2017

SOKA LINALIPA MWANANGU, LINGARD MIEZI 18 MAN UNITED, SASA ANA GARI LA SH MILIONI 500.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Jesse Lingard sasa ana miezi 18 tu ndani ya kikosi cha Manchester United na mafanikio ya kimaisha yameanza kuonekana.
Umri wake ni miaka 24 tu, tayari sasa anamiliki gari la kifahari aina ya Bentley Continental GT lenye thamani ya pauni 200,000 (zaidi ya Sh milioni 545.2)
Hii inaonyesha kiasi gain mchezo wa soka unavyoweza kulipa. Kama una kipaji ni vizuri kukitumia kwa ajili ya mafanikio.
Kwa wachezaji wa nyumbani Tanzania, inawezekana vigumu kufikia kununua gari la Lingard, lakini soka ni mchezo unaoweza kuwa ajira itakayobadilisha maisha yako. Inategemea kiasi gani uko makini katika kazi yako.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment