Thursday 30 March 2017

Jide Afunguka ya Kuachwa na Mnigeria Wake.Fahamu zaidi hapa.

Jide afunguka ya kuachwa na Mnigeria wake

Wakati maneno ya chini chini yakiwa yanaendelea kuhusu kupigwa kibuti na mpenzi wake mpya Spicy kutoka Nigeria, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ amefunguka na kusema wabongo wengi wanapenda wenzao waharibikiwe na kuwataka kuacha kuwaziana mabaya.

Jide amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya maneno kuzagaa kuwa amepigana kibuti na Mnigeria huyo ikiwa ni siku wiki chache baada ya kuandika maneno yaliyomo kwenye wimbo wa  Rosella katika mtandao wa Instagram.

“Niko vizuri na Spicy, yale maneno niliandika kwa ajili ya muziki, watu wanapenda kuona wenzao wanaharibikiwa, kwanini wanakimbilia kuamini nina matatizo na Spicy na hawafikirii kuhusu kazi yangu? Niwakaribishe waje kwenye show yangu ya uzinduzi pale Lugalo Uwanja wa Gofu Ijumaa hii,” alisema Jide.
Lady Jaydee anayetamba na wimbo wa Rosella alioshirikiana na h_art the band kutoka Kenya anatarajiwa kuzindua albamu yake ya saba tarehe 31 ya mwezi huu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment