Tuesday 28 March 2017

RONALDO AMPIGA BAO LIONEL MESSI KWA KIPATO HADI SASA, NEYMAR AMUACHA BALE.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameongoza kwa kuwa mwanasoka mwenye kipato zaidi kwa msimu wa 2016-17 hadi sasa.

Ronaldo tayari ameingiza kitita cha pauni milioni 75.62 na amempiga bao mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Barcelona ambaye amepata pauni milioni 66.12.

Fedha hizo zinatokana na mshahara, posho, malipo ya motisha na mikataba ya matangazo na Ronaldo anaonekana amepanda haraka baada ya kushinda Ballond'Or.

Kiungo mwingine wa Barcelona, Neymar, yeye anaonekana kumpiga bao Gareth Bale wa Madrid.

Listi hii hapa



MCHEZAJI                               TIMU                            KIPATO
Cristiano Ronaldo            Real Madrid           Pauni 75.62m
Lionel Messi                    Barcelona           Pauni 66.12m
Neymar                                    Barcelona                   Pauni 47.97m
Gareth Bale                            Real Madrid   Pauni 35.4m
Ezequiel Lavezzi              Hebei China                Pauni 24.63m


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment