Monday 3 July 2017

JERRY Muro Amtupia Haji Manara Kijembe Hichi Baada ya Kumaliza Kifungo cha TFF, Adai Maisha ni Gwaride.

Aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Jerry Muro amemaliza kutumikia adhabu yake.


Jerry alifungiwa mwaka jana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TTF) kwa mwaka mzima kutojihusisha na shughuli zozote za kimichezo kutoka na utovu wa nidhamu. Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram hiyo jana usiku Jerry aliandika haya machache.

Natabasamu kwa kuwa Leo 02/07/2017, nimemaliza kutumikia Adhabu “DHALIMU” Kikombe nilichonywea mimi na wao wamekipokea wanaanza kunywea humo, Maisha ni kama Gwaride Kiongozi akisema Nyumaa Geuka wa mbele anakuwa wa MWISHO na wa mwisho anakuwa wa KWANZA, Vumilia ndugu YANGU @hajismanara nakuaubiria “USWAHILINI” Kaeni tayari kwa ujio Mpya @yangasc@simbasc @azamfc

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment