Kocha mzawa ambae ameiongoza timu ya taifa kwa muda mrefu Chalres Boniface Mkwassa, sasa hivi sio tena kocha wa timu yetu ya taifa.
Rais wa TFF ndugu Jamal Malinzi kupitia ukurasa wa twitter ametoa taarifa inayosomeka: “Mkataba wa TFF na Kocha Mkwassa, umefikia mwisho leo kwa makubaliano. Salum Mayanga ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa muda wa Taifa Stars”.
Ikumbukwe kamba kocha huyu alichukua mikoba kutoka kwa kocha Mart Nooij raia wa Uholanzi ambae alifundisha tangu mwaka 2014 hadi 2015.
Endelea kufatilia shaffihdauda website utajua zaidi kuhusu kusitishwa kwa mkataba huu na sababu zake kama zitawekwa wazi na moja kati ya pande hizi mbili.
Hii hapa chini ni taarifa rasmi ya TFF kuhusu hatma ya Mkwasa kuifundisha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua Salum Mayanga kuwa kocha wa muda (Interim coach), wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’.
Kocha Salum Mayanga anachukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi Machi, mwaka huu – 2017.
Kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.
Pia Kocha Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).
TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment