Mwanamuziki Z-Anto ambaye aliwahi kufanya vyema katika muziki miaka ya
nyuma na kuamua kukaa pembeni huku akifanya biashara zake ameanza vyema
mwaka 2017 kwa kujenga nyumba ya nne nje ya kazi yake ya sanaa.
Z-Anto ambaye makazi na shughuli zake za
kila siku zipo Kigamboni Dar es Salaam, amefunguka na kusema ameamua
kuanza mwaka 2017 kwa kujenga nyumba yake ya nne ambazo amejenga nje ya
kazi yake ya muziki na sanaa kiujumla.
"Wiki mbili za mwanzo za mwaka 2017. House namba 4. Mwaka ndivyo tulivyouanza. #Thnxgod nje ya sanaa" aliandika Z Anto
Z-Anto mwaka kupitia kipindi cha Planet
Bongo aliahidi kurudi kwenye muziki na kusema kuwa label mbalimbali
kubwa nchini zaidi ya nne zimemfuata ili wafanye kazi na kusema yeye
anahitaji kuchanganua ili ajue ni label ipi ambayo inaweza kumpeleka
mbali kimuziki na kufikia malengo yake kwenye muziki.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment